banner

.

.

Friday 11 August 2017

HUU NDIO MUONEKANO HALISI WA WA ALBAMU YA MWAHANGILA..

Kwa muda mrefu Christopher Mwahangila amekuwa akifanya vizuri sokoni kupitia albamu yake ya Mungu ni Mungu Tu lakini siku ya jana kwenye ukurasa wake wa Facebook anaotumia kwa jina la Chriss Mwahangila amepost picha inayoonyesha muonekano wa kava la albamu yake mpya iitwayo "Mungu hawezi kukusahau"
Kwenye cover hilo kwa juu kuna maneno ya wimbo uliobeba albamu yaliyoandikwa MUNGU HAWEZI kukusahau kuna picha yake kubwa inayoonyesha kuwa yeye ndiye mmiliki wa hii album kuna Stika ya TRA kuhakikisha kwamba hii ni kazi Original na sio fake kuna Mawasiliano ya Msambazaji wa hii albamu ambao ni Mbogo Production kuna Jina lake la Christopher Mwahangila na chini kuna mawasiliano yake...Albamu ya Christopher Mwahangila iitwayo Mungu Hawezi Kukusahau sasa inapatikana madukani kote....

Tupe maoni yako