banner

.

.

Thursday 23 January 2014

ROSE MUHANDO KUACHIA ALBAMU MPYA YA YESU KUNG,UTA{ WOLOLO} MWEZI WA PILI 2014...

Mwimbaji nguli wa Muziki wa Injili nchini Tanzania Rose Muhando anatariji kuachia albam yake mpya mwezi wa pili mwaka huu chini ya mkataba na kampuni ya kimataifa ya Sony.

Akizungumza na mtandao wa www.matukiomedia.blogspot.com Rose Muhandao amesema kuwa albamu yake mpya itakuwa na nyimbo nane ambazo zimerekodiwa kisasa zaidi katika studio za kimataifa nchini Afrika Kusini.

Amesema katika albamu hiyo ameimba mahadhi ya aina mbalimbali ili kuleta ladha nzuri kwa wapenzi wake. Pia ameweka wazi kuwa kwa sasa yuko chini ya Sony, hivyo kila Mtu akayemwihitaji lazima awasiliane na Sony ili aweze kupatikana kwa huduma.

Kuhusu kuimba live Rose amesema kuwa yeye kwa sasa ndo mtindo anaoutumia na kila atakaposimama steji wapenzi wake wategemee kupata ladha halisi kutoka kwake.

Mpaka sasa Rose Muhando ana albamu sita ambazo ni:
1. Mteule uwe Macho.
2. Jipange Sawasawa.
3. Nyota ya Ajabu.
4. Utamu wa Yesu.
5. Mungu Anacheka.
6. Yesu Kung'uta ambayo ndo mpya inayokuja.

Mtandao wa www.matukimedia.blogspot.com unampa big up kwa kazi kubwa anayoifanya hasa kupeleka injili mbele na kuwaleta watu kwa Yesu.





Tupe maoni yako