banner

.

.

Friday 7 March 2014

AJALI ILIYOUA NA KUJERUHI MAKUMI YA WATU MOROGORO..


Zifuatazo ni picha za ajali iliyohusisha magari matatu siku ya Alhamisi, (6 Machi 2014) eneo la Bwawani, barabara kuu iendayo Morogoro, ambapo gari la mafuta aina ya Iveco lenye namba za usajili T272 ASB, mali ya kampuni ya OilCom imeripotiwa kugongana uso kwa uso na gari la abiria, Tata, Linowele Classic lenye namba za usajili T252CHN lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Malinyi pamoja na gari nyingine ya abiria la Adventure, lenye namba za usajili T335CCD, Nissan Diesel iliyoripotiwa kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kigoma.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wanaeleza kuwa ni mwendo wa gari la Linowele, ambapo dereva wake alishindwa kuumudu kutokana na mvua zilizokuwa zinanyesha, na hivyo kupelekea kulivaa lori la mafuta, ambapo dereva wa lori amefariki dunia. Kwa upande wake, dereva wa basi la Linowele ameripotiwa kubanwa na usukani na kupelekea kuvunjika mguu, ambapo askari magereza walifanikiwa kutoa msaada mkubwa kwa majeruhi wanaoripotiwa kufikia 38.

Kwa maelezo ya mashuhuda, basi la adventure nalo wakati likija kwa mwendo kasi kukaribia eneo la tukio, jitihada zilifanywa na askari kulisimamisha ili lisipate kuyavaa magari hayo mawili, ambapo kuona hivyo, dereva wake alilazimika kukwepesha na kisha kuliingiza mtaroni. Zifuatazo ni picha za tukio lote, kama ambavyo GK ilifanikiwa kufika eneo hilo.





Wananchi wakitazama mabaki ya gari la abiria, Linowene iliyokuwa ikielekea Malinyi, Morogoro kutokea Dar es Salaam.




Dereva wa lori, Scania, mali ya kampuni ya Twiga Cement akijiandaa kuvuta gari la Linowene, kabla ya kuachia kijiti kwa lori lingine kuiyuta kwa pembeni, nje ya barabara.




Taswira kwa mbali ikionyesha basi la Linowele na Adveture, ambapo lori aina ya Scania likiivuta kuiondoa barabarani

Mwili wa dereva wa gari la mafuta, mali ya kampuni ya OilCom.




Sehemu ya foleni kwenye eneo la tukio.
Picha na Gk Blog

Tupe maoni yako