banner

.

.

Friday 11 August 2017

WOLPER KUSAPOTI MZIKI WA INJILI...

Mwigizaji maarufu wa filamu za kitanzania Jackline Wolper anatarajiwa kuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa wanaotarajiwa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa album ya Mwimbaji wa muziki Injili Magreth Sembuche iitwayo Waambie Wataabishaji,


Tamasha la uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili hii ya tarehe 13-8-2017 kwenye ukumbi wa kanisa la Angilikana lililopo Salasala, Mbezi Beach kuanzia saa saba mchana na kuendelea,
Pia waimbaji mbali mbali watakuwepo wa muziki wa injili watakuwepo kumsindikiza Magreth Sembuche katika uzinduzi wake kama Masanja Mkandamizaji, Christopher Mwahangila, Tumaini Njole, Edson Mwasabwite, Mc Joshua Makondeko na wengine kibao kwa Mawasiliano zaidi 0717163146.

Tupe maoni yako