banner

.

.

Friday 7 July 2017

SANCHEZ APEWA MAKAVU NA SHABIKI WA ARSENAL JUU YA MSHAHARA WAKE

Suala la Sanchez kubaki au kuondoka Arsenal bado ni kizungumkuti kwani hadi sasa mkataba mpya haujasainiwa na wala haieleweki kwamba mazungumzo yanaendelea au laa.
Tetesi zinasema Sanchez yuko tayari kubaki katika klabu ya Arsenal lakini apewe £400,000 kwa wiki!suala ambalo linaonekana ni gumu sana kutokea katika klabu ya Arsenal.
Ni ngumu sana kumpa mkataba mpya utakaomfanya apokee kiasi cha€400,000 haswa kwa mchezaji ambaye umri wake umevuka miaka 27, kwanza sio ngumu ila haiwezekani.
Kwanza ona ligi nzima ya Bundesliga hakuna mchezaji anayelipwa £200,000 kwa wiki, ni Lewandoski peke yake anaelipwa mshahara mkubwa nao ni £180,000 kwa wiki, Sanchez pesa anayotaka ni kichekesho.
Eden Harzad mchezaji ambaye aliidharilisha Arsenal aliyipo Sanchez kwa kuifunga moja ya mabao bora kabisa kuwahi kufungwa msimu uliopoua analipwa £200,000 kwa wiki pamoja nakuchukua Epl lakini bado hajaomba kuongezewa mshahara
Cristiano Ronaldo mchezaji bora wa dunia analipwa £360,000 kwa wiki, unataka kulipwa hela nyingi kumzidi hata mchezaji aliyechukua kombe kubwa kama Champions League na La Liga?
Neymar pamoja na umri wake wa miaka25 na kiwango kikubwa sana huku miguu yake ikijaa udambwi mwingi lakini analipwa £250,000 sasa Sanchez anamzidi nini haswa mpaka hata £300,000 wanayokupa Gunners?
Douglas Costa analipwa £100,000 kwa wiki pamoja na ufundi wake wote, Sanchez si ulikuwemo wakati mnapunyuliwa 10-2 AGG na Bayern?  Douglas Costa hasemi anataka £300,000 kwa wiki pamoja na upambanaji wake wote, ila wewe uliyefungwa 10 unadai kiasi hicho?
Sio Chelsea wala Man City wala Man U, wala Barcelona, wala Bayern, wala PSG wala Madrid  hakuna mchezaji anaelipwa £400,000 kwa wiki sasa sisi leo Arsenal ndio tukupe £400,000? Hapana kwakweli hizo ni bangi kama hututaki wewe nenda tu kanza tuna Lacazatte.

Tupe maoni yako