banner

.

.

Friday, 7 July 2017

STARS YAIBUKA MSHINDI WA TATU MICHUANO YA COSAFA.

Timu ya Taifa Stars ya Tanzania yapambana kuisaka nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini na hii ni baada ya kutolewa katika nusu fainali bada ya kufungwa mabao manne na timu ya Zambi, Nahivyo kupelekea kukutana na timu ya Lesotho ambayo ilifungwa na Zimbabwe mabao 4-3. Hivyo timu zote mbili zimekutana kila moja ikiwa imepoteza mchezo wake nusu fainali, katika mchezo wa leo kila timu ilikuwa ikicheza kwa tahadhari kubwa na kufanya mashambulizi ya kushitukiza hata hivyo mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika kulikuwa hakuna timu ambayo iliweza kutikisa nyavu za lango za mwenzake kwani milango yote ilionekana kuwa migumu kwa timu zote mbili licha ya timu hizo kupoteza nafasi za wazi katika mchezo huo.

Tanzania Inaibuka Washindi wa Tatu wa Michuano ya Cosafa 2017 baada ya Kushinda kwa Penati 4 kwa 2. Waliofunga Penati zao ni Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Alpha huku Kichuya Akikosa Penati ya Kwanza Kabisa.

Tupe maoni yako