banner

.

.

Wednesday 19 July 2017

ANTONIO CONTE ASHUSHA PUMZI KWA KUPATA MKATABA WA MIAKA 2 KUIFUNDISHA CHELSEA.



London, England. Baada ya kuwa katika sintofahamu kwa muda mrefu, hatimaye Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho.
Awali, Conte alikuwa akihusishwa kurudi Italia katika msimu huu wa usajili wa kiangazi, hivyo mkataba huo mpya umemaliza tetesi hizo zilizokuwa zikiripotiwa kwenye vyombo vya habari.
Kocha huyo amesajiliwa kwa mkataba wa thamani ya Pauni 20 milioni.
Conte alisema ni jambo la furaha kwake kuongezewa mkataba na anaamini mafanikio yake aliyoyapata katika mwaka wake wa kwanza akiwa Chelsea ndiyo yamewasukuma mabosi wake kumbakiza klabuni hapo.

Tupe maoni yako