Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ yazidi kuwapa watanzania wengi faraja
- Yatoa zaidi ya shilingi milioni 194 kwa washindi
- Tiketi 18 za kwenda Old Trafford zatolewa
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel
Tanzania imeendelea kuwapa faraja washindi wake wa promosheni ya ‘Mimi
ni Bingwa’ kwa kuwazawadia zaidi ya pesa taslim shilingi milioni 194 na
kutoa tiketi 18 za safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old
Trafford nchini Uingereza.
Kampuni hiyo ya mawasiliano jana imetoa
shilingi milioni 22 pesa taslim kwa washindi 14 na tiketi mbili za
kwenda Old Trafford kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa
moja ‘live’, kwa mshindi mmoja wa kila wiki katika wiki ya tisa ya
promosheni ya Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa katika ofizi ya makao makuu
ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya droo, Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema promosheni ya Mimi
ni Bingwa imekuwa ikiwapa faraja watanzania wengi ambao wamekuwa
wakionyesha furaha zao za ushindi wa pesa taslim au safari
inayogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford.
“Tumekuwa tukipokea maoni kutoka kwa
washindi wetu, hususani wale waliojishindia pesa taslim, wakisema pesa
waliojishindia toka promosheni ya Mimi ni Bingwa wameipata wakati
muafaka wakihitaji zaidi msaada wa kifedha.
“Wanasema
miezi iliyochaguliwa kwa ajili ya promosheni na pesa walizopokea bila
jasho kutoka Mimi ni Bingwa promosheni, zimeweza kuwaongezea uwezo wa
kifedha ili kupambana na hali ngumu ya kiuchumi katika miezi hii migumu
inayohitaji fedha nyingi. Tumekuwa tukituma milioni moja (1m/-) kwa
washindi wetu mara tu baada ya kuwatangaza kupitia Airtel money na
kuweka shilingi milioni tano (5m/-) katika akaunti za washindi baada ya
kupata taarifa zao za benki,” alisema Mmbando.
Aliongeza kuwa promosheni hiyo ya Mimi ni
Bingwa iliyoanza mwishoni mwa mwezi wa Novemba mwaka jana, imelenga
kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa jamii inayoizunguka na
kuwaunganisha mashabiki wa soka na michezo ya kimataifa.
Alimtangaza Edwin Edmund Kajimbo kutoka
Iringa kuwa ni mshindi wa wiki hii wa tiketi mbili wa safari
iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi za klabu ya
Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.
Bw. Kajimbo anakuwa ni mshindi wa tisa wa
tiketi toka promosheni ilipoanza baada ya Michael Joseph Shirima kutoka
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mwenyekiti wa
Kijiji cha Nang’olo katika wilaya ya Kilwa - Mkoani Lindi, Leonard
Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar
es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro mkoani Arusha, Rashid
Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo
kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Juma Mughery kutoka Dar es
Salaam, waliojishindia tiketi katika droo za kila wiki zilizopita.
Mmbando
pia aliwatangaza washindi wawili wa shilingi milioni 5 kila mmoja wa
wiki kuwa ni Bw. Uruma Samwel Mkongwa kutoka Usa River mkoani Arusha na
Filemon Nathaniel Mgaya kutoka Dar es Salaam pamoja na washindi wengine
10 waliojishindia shilingi milioni 1 kila mmoja.
“Zaidi ya shilingi milioni 324 zilitengwa
kama zawadi ya pesa taslim kwa ajili ya promosheni ya Airtel ya Mimi ni
Bingwa, inayowapa fursa washiriki wa Mimi ni Bingwa kushinda kila siku
na kila wiki,” alisema.
Mmbando alisema kuwa mwenendo wa washiriki wa Mimi ni Bingwa kuendelea kujikusanyia pointi unazidi kutoa amasa.
“Bado
kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa
ya shilingi milioni 50. Nawaasa wateja wa Airtel ambao bado
hawajajisajili katika promosheni hii kuwa hawajachelewa; bado kuna
zawadi nyingi zaidi kushindaniwa. Ili kuingia katika promosheni hii
mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BNGWA” kwenda
namba 15656, kwa kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza kuwa mshindi
wa milioni 50 au zawadi nyinginezo nyingi,” alisema.
Tupe maoni yako


