Na: JACKTAN MSAFIRI
Mwanza.
Ni kijana mwenye umri wa miaka
17 mwenye kipaji cha hali ya juu katika kusakata kandanda ambaye anadai urasimu
uliokithili wa viongozi katika kabumbu ndio chanzo cha kupoteza vipaji vya
vijana
Akizungmza na mtandao wa www.matukiomedia.blogspot.com
hii katula
amesema viongozi wenye dhamana sio ngazi kubwa hadi ndogo wamekuwa wenye
kujinufaisha wao na vizazi vyao huku ubaguzi na upendeleo ukitawala katika club
mbalimbali navyama vya soka hasa wilayani.
“Mimi nimeshiriki katika ligi
mbalimbali za vijana ikiwemo kopa cocacola lakini ilifika sehemu nikaachwa kwa
kuwa sikuwa na laki moja ya kutoa ili nijumuishwe katika ngazi ya taifa na walioweza
kutoa waliendelea, kweli mkono mtupu haulambwi” alisema katula
Kijana huyo amesema kuwa kitu
kingine kinachoporomosha soka la vijana ni kukosekana kwa shule za kuibua
vipaji yaani academy,kukosekana kwa vifaa vya michezo na viwanja na uhaba wa
ligi za vijana
Anasema “mimi ningekuwa raisi
wa tff ningeanza kwa kurekebisha ligi kuu kwa kuongeza idadi ya timu angalau
zifike 18 ili kuongeza ushindani na ningeongeza idadi ya ligi bila kusahau
kuwekeza kwa hali ya juu katika soka la vijana”
Coolwizzila katula ndimmila(17)amezaliwa
mjini nansio wilayani ukerewe katika mkoa wa mwanza,klabu alizowahi kuchezea ni
nansio utd,kagera fc na muungano fc zote za wilayani ukerewe
Nafasi anazocheza uwanjani ni
kiungo mshambuliaji na winga na jumla ya mechi rasmi alizocheza ni 109 akifunga
magoli 65 ambapo malengo yake ni kucheza mpira wa kulipwa hasa nchini uingereza
ambapo amesema anafanya kila liwezekanalo kuhakikisha anafanikisha malengo yake.
Alipo ulizwa kwa nini amechagua
kandanda kati ya michezo yote amesema “mbali na kuwa na kipaji mchezo huu upo
kwenye damu,na nimewahi kulala mtaani vibalazani baada ya kukosa mwenyeji
nilipoenda kucheza fainali ya kombe la mbuzi katika wilaya ya kwimba ila sikuumia
kwa kuwa nilijua najenga ndoto zangu na nilifunga magoli 3 peke yangu ambayo
yaliipa ushindi timu yangu”
Mchezaji anayemkubali kwa hapa
Tanzania ni mlisho ngassa na ulaya
anamkubali sana Didier drogba.Katula amewaomba
watu wenye uwezo wa kuendeleza ndoto zake wajitokeze kufanya hivyo kwa
kuwasiliana na uongozi wa safu hii au kwa simu yake ya mkononi 0762646746
Tupe maoni yako



