![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mary Tesha akitaka maelekezo kutoka kwenye kabrasha la Kikao hicho (Kulia) na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Jackiline Liana na Mkuu wa Wilaya Ilemela Amina Masenza |
![]() |
| Sehemu ya Wajumbe ambao ni Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Mwanza |
![]() |
| Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Hassan Hida |
![]() |
| Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor akitaka ufafanuzi juu ya ujenzi wa kiwango cha lami kutoka Hungumalwa kupitia Mwankurwe, Nyamilama, Ngudu hadi Magu. |
![]() |
| Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Eng. Leonard Kadashi akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe wa kikao hicho kinachoendelea sasa. |
![]() |
| Mwenyekiti wa Kikao Eng. Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) akisisitiza jambo kwenye kikao. |
![]() |
| Ndani ya Kikao Ukumbi wa BOT Mwanza. |
Akizungumza
katika kikao cha Bodi hiyo kilihofanyika leo kwenye chuo cha Benki Kuu
ya Tanzania (BOT) Kapiripoint jijini hapa, Mwenyekiti wa kikao hicho,
mhandisi Evarist Ndikilo ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, ameagiza
Meneja huyo ‘alimwe’ barua ya onyo na nakala yake apewe Waziri wa
Ujenzi.
Ndikilo alisema kwamba, Meneja huyo
ameshindwa kutekeleza maazimio ya kikao kilichopita cha Bodi hiyo kwa
muda wa mwaka mzima sasa na kukacha kikao cha jana bila majibu sahihi ya
utekelezaji, hali inayoonyesha amekidharau kikao hicho.
Aliyataja maagizo hayo kuwa ni kuweka
choo katika kivuko cha MV Kome II kinachotoa huduma kati ya Nyakarilo na
kisiwani Kome wilayani Sengerema na kutoa elimu ya matumizi ya vifaa
vya kujikololea kwa abiria wa vivuko vyake vyote mkoani humo.
Agizo jingine ni kuwanunulia sare
wafanyakazi wa vivuko hivyo ambao inadaiwa wengi wao wamezigomea baada
ya kutakiwa wakatwe gharama ya sare hizo kwenye mishahara yao.
“Temesa
wamedharau agizo la Bodi hii tulilolitoa mwaka mzima uliopita, Meneja
wake aandikiwe barua ya onyo na RAS na kutakiwa kutoa majibu ya
utekelezaji wa maagizo hayo katika kikao kijacho.” Alichachamaa Ndikilo
na kuagiza nakala ya barua hiyo ya onyo ipelekwe kwa Waziri wake wa
Ujenzi, John Mgufuli.
Hatua hiyo ilitokana na Kaimu Meneja wa
Temesa Dauson Nyonyi kushindwa kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu
utekelezaji wa maagizo hayo alipoeleza kuwa, mkandarasi hajaweka choo
hicho katika kivuko cha Kome II liha ya kutakiwa kukamilika mwishoni mwa
mwaka jana.
Nyonyi
alisema, TEMESA imeweka kanda za CD katika vivuko vyake ambazo
zinaonyesha namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea vikiwemo Life Jacket
na kuwanunulia sare wafanyakazi wa vivuko vyake vyote bila lakini baadhi
ya wajumbe walikataa kuwa taarifa hiyo ya TEMESA si sahihi.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la
Buchosa ndiye aliyeanza kupinga utekelezaji wa maagizo hayo alipodai
kuwa mkandarasi Songoro Marine Transport, toka mwaka jana ametengeneza
choo hicho lakini hadi sasa Meneja wa TEMESA hataenda kukihukua na hana
mawasiliano na Songoro.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Joseph Mkundi, alisema majibu ya
Nyoni si sahihi kwani sare hizo zimenunuliwa lakini hazijagawiwa kwa
wafanyakazi kutokana na kutakiwa kukatwa garama ya nguo hizo katika
mishahara yao na hivyo kuwafanya wazisusie.
Mkuu
wa wilaya ya Sengerema, Karen Yunus alikiambia kikao hicho kwamba,
TEMESA ni waongo, hawajatoa mafunzo yoyote ya matumizi ya vifaa vya
kujiokolea kwa wateja wao (abiria) na hawajawapa sare huku akisisitiza
kuwa wanapaswa kupewa sare hizo bila kukatwa katika mishahara yao.
Pamoja
na michango ya wajumbe wengine, kikao hicho kilikataa majibu ya TEMESA
na kudai kuwa ni blablaa tu kinataka kuona utekelezaji kwa vitendo na
pamoja na kumpa onyo Senkoro, kilimuagiza atekeleze haraka maagizo hayo.
Tupe maoni yako










