Siku
ya leo macho na masikio ya watanzania hasa wafuasi na wapenzi wa
chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA) yalielekezwa katika
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo
Jaji John Utumwa alikuwa akitoa hukumu dhidi ya kesi ya Zitto
Kabwe na uongozi wa juu wa CHADEMA.
Zitto
ambaye alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi
katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho
iliyokutana tarehe 3 na 4 mwezi huu kujadili hatima ya
uanachama wake wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake ya
kupinga kuvuliwa nyadhifa zake zote za uongozi ndani ya chama
hicho...
Akisoma hukumu ya kesi hiyo baada ya kuiahirisha jana, Jaji wa mahakama hiyo,Jaji
Utamwa ameridhia pingamizi lililotolewa na mh. Zitto Kabwe la
kutojadili uanachama wake na kuitaka kamati kuu ya CHADEMA au
chombo kingine chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi
yake ya msingi ( rufaa ) itakaposikilizwa na baraza kuu la
chama hicho.
Tupe maoni yako

