
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi hundi kwa washindi watatu waliopewa dola 25,000 kila mmoja chini ya mradi wa Tigo Reach for Change.
Tigo leo imechagua na kutangaza washindi watatu watakaopewa dola 25,000 kila mmoja chini ya mradi wa Tigo Reach for Change uliozinduliwa mwezi Novemba mwaka jana yenye malengo ya kuboresha maisha ya watoto nchini.
Wajasiriliamali jamii hao watatu walioshinda ni:
1.Faraja Nyalandu, na mradi wa Shule Direct;
'Shule Direct' ina malengo yakuhamasisha na kuhakikisha kwamba mtaala bora ya elimu inapatikana kidigitali kiurahisi na kwa ufanisi zaidi kupitia njia ya simu za mkononi (SMS na kwa kupiga) kwa ajili ya maendeleo mema ya wanafunzi wakitanzania.
2. Joan Avit na mradi wa GraphoGame Tanzania;
'GraphoGame' ni mchezo wa watoto uliowekwa kwenye mfumo wa kompyuta (apps) inayoweza kutumika kwa njia ya simu yenye malengo ya kuwawezesha watoto kujua kusoma na kuandika. Imewekwa kwa njia ya mchezo ili kuweza kuwa fanisi zaidi kwa kuwafurahisha na kuwashirikisha watoto pindi wanapokuwa wanajifunza.
3. Carolyne Ekyarisiima na mradi wa Apps and Girls;
'Apps and Girls' ina malengo ya kuwahamasisha wasichana na wanawake kuweza kuelimika zaidi katika masuala ya Teknohama.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman akielezea jinsi walivyoendesha zoezi la kuchagua mawazo yaliyotumwa na watu zaidi ya 1000.
Tupe maoni yako
