banner

.

.

Sunday 2 February 2014

WAKRISTO WAKUMBUSHWA KUTOKUTEGEMEA AKILI YA KIBINADAMU, BALI WATEGEMEE AKILI ZA MUNGU.

 Mchungaji wa Kanisa la The Pool of Siloam Nehemia Conqueror Eliya akifundisha katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika ukumbi wa Vijana Social ambapo amegusia wakristo kutotegemea akili zao bali wamtegemee Mungu pekee yake.
 Umati mkubwa wa Wakristo ambao ni washarika katika Kanisa hilo wakiimba na kumshangilia Mungu wakati wa ibada ya sifa kanisani hapo.
 Bwana harusi Nafsi Hai Conqueror Eliya akiwa na bibi harusi Agano la Nuru Conqueror Eliya wakiwa na nyuso za furaha wakati wa ibada ya ndoa yao iliyofanyika leo katika kanisa la Siloam linalofanyia ibada zake katika ukumbi wa Vijana Social Mwanza
    Bwana na Bibi Harusi wakimachi kwenda madhabahuni kwa ajili ya ufungishwaji ndoa.
                      Msafara wa Maharusi kama inavyoonekana pichaniii.
                Taswira halisi za maharusi kama wanavyoonekana kwa mnato huo.
 Mwonekano wa maharusi katika ibada ya kufungishwa ndoa ili wawe mtu na mke wake kuanzia leo na kuendelea.
 Washarika wa kanisa la Siloamu...wakiwa wamevaa mavazi white... Vazi la Malaikaa
Kila msharika akidance  staili yake anayoiweza wakati wa kipindi cha  sifa kikiendelea mbele za Mungu kama picha za Matukio Media Blog ilivyowakamata.

WAKRISTO wote waamekumbushwa kutokutegemea akili zao bali kizitegemea akili za Mungu ali waweze kupata majawabu mazuri kutoka kwa Mungu na ndipo watakapojua utendaji wa Mungu ambao hutokana na uweza wake.

Hayo yamesemwa na Mchungaji Nehemia Conqueror Eliya katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika ukumbi wa Vijana Social ambapo kanisa la Siloam hufanyia ibaada zake na kuhudhuriwa na mamia wa wakristo kutoka Mwanza na Mikoa ya Jirani.

Mchungaji Eliya amesema kuwa baadhi ya wakristo wamekuwa wakitumia akili zao ambazo hazina matokeo mazuri ambazo hupelekea kushindwa kuziona baraka timilifu kutoka kwa Mungu baba ambae ndiye mtoaji wa kila kitu.

Amesema hata kipindi cha mababu zetu wengi wao walitegemea akili za mababu ambazo walikuwa wakitoa kafara ambazo hakuwa na maana yoyote kwa mizimu na hawakupata matokeo ambayo waliyatarajia kuyapata kutoka kwa mizimu.

Sanjari na hayo ametoa mwito wakristo na Serikali  kutokutegema misaada kutoka nje ambayo hatujui inatoka na masharti gani. Pia amewaasa vijana kutokutemegemea kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo yao bali wajikite kujiajiri na kutegeneza fursa ya kuwa na vipato vya uhakika.

Katika ibada hiyo pia ilifanyika harusi ya Bwana Nafsi Hai Conqueror Eliya na Bibi Agano la Nuru Conqueror Eliya ambapo walifungishwa ndoa ili waanze kuishi kama mke na mme maana ndio mpango wa Mungu kuwa hivyo.


Tupe maoni yako