banner

.

.

Monday 3 February 2014

SAMUEL LUSEKELO: NAKUJA MWANZA PASAKA KUWAPA RAHA MASHABIKI WA MUZIKI WA INJILI.

       Samuel Lusekelo akiwa katka shot mojawapo katika albam yake iitwayo Tunza Kibali.
Akiwa nyumbani hupenda kukumbatia mbwa wake akiwa ni moja kati ya mambo anayoyapenda maishani mwake.

 "Nakuja Mwanza kuwapa raha mashabiki na wapenzi wa Muziki wa Injili na hii namaanisha kwamba Pasaka hii lazima kitaeleweka"

Haya ni maneno yake Mwimbaji Nguli wa Nyimbo za injili Lusekelo Samuel Mwaitalako ambaye alianza kuongea wakati akifanya mahojiano na mtandao wa www.matukiomedia.blogspot.com.

Lusekelo anasema kuwa toka akiwa kijana mdogo alikuwa akitamani kuja kuimba katika steji kubwa sana na yenye watu wengi na kwa sasa anamshukuru Mungu kwa kufungua mlango wa kuimba katika matamasha makubwa kama yanayoandaliwa kwa sasa nchini.

"Zamani hatukuwa na fursa ya kuimba katika matamasha makubwa kama ya leo, kipindi cha nyuma kulikuwepo na mikutano na matamasha madogo madogo ili kwa sasa kuwa matamasha makubwa ya kimataifa yanayoandaliwa na makampuni mbalimbali ili kuinua vipaji vya waimbaji wa muziki wa injili hapa Tanzania".

Lusekelo mwimbaji na mwanamuziki mkubwa nchini Tanzania ambaye ameanza kuimba toka utotoni na kukuza kipaji chake chini ya Mwalimu wake Daudi Ngao amabe alimlea na kumwingiza kwenye kwaya. .

Baada ya kukuingia kwenye kwaya niliimba na hatimaye nikajiunga na Ephraim Mwansasu kwa Miaka miwili na kuanza kusimama mimi kama mimi kwa msaada wa Mungu.

Ingawa nilikuta game ya Muziki wa Injili ni gumu nilijitahidi hatimaye nikakamilisha kutengeneza albam yangu ya kwanza ya Tunza Kibali ambayo ilipokelewa kwa na mashabiki kwa mikono miwili. Baadae nilirekodi albam ya pili iitwayo Imeandikwa.

Amezitaja changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha harakati ya muziki wa Injili usisonge mbele zaidi kama sapoti kutoka kwa wadau na wapenzi wa muziki huo, baadhi ya watumishi wa Mungu kutotoa nafasi na fursa ya kutosha kuhudumu na kutokuwa na wasambazaji wengi wa kusambaza kazi za waimbaji.

Ametaja mafanikio aliyoyapata mpaka sasa ni kwenda maeneo mbalimbali kutumika, kufahamiana na waimbaji mbalimbali na watumishi wa Mungu. Pia kurekodi albam mbili za kiwango cha juu.

Katika kila kuna mtu unayempenda, Lusekelo anasema anampenda sana mwimbaji Emmanuel Mgogo kutoka Mbeya kwa upande wa wanaume na kwa upande wa wanawake anamhusudu Deborah Mwaisabila. Nje ya Tanzania anampenda sana Benjamin Dude kutoka Afrika Kusini.

Lusekelo amewaomba wakereketwa na wapenzi wa Muziki wa Injili kumpata sapoti na pia kuwaasa kumshauri na kumwelekeza ili afanye vizuri zaidi katika tasnia ya Muziki.

Sanjari na hayo amewaomba wakazi wote wa kanda ya ziwa na mikoa jirani kujitokeza katika tamasha la Gospel Festival 2014 CCM Kirumba 20/4/2014 na 21/4/2014 ili waje waone kile anachokisema kuhusu uimbaji wake. Zaidi ya yote napenda kuimba live zaidi kuliko cd.


Tupe maoni yako