banner

.

.

Thursday, 27 February 2014

MADINI AINA YA TANZANITE YANGA’RA BANGKOK..


1Baadhi ya madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana katika mabanda mbalimbali katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok Gems and Jewelry Fair.2Mfanyabiashara  wa madini na Afisa Masoko wa Kampuni ya Tom Gems Tanzania, akimwonesha mgeni aliyefika katika banda la Tanzania kuona madini ghafi ya Tanzanite  yanayozalishwa Tanzania pekee. Wageni wengi wamefika katika banda hilo kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania.3 (2)Mwenyekiti wa Madini ya Viwandani Bw. Kassim Iddi Pazi, akimwonesha mgeni madini ya Ruby. Kutokana na maelezo ya Bw. Pazi, ameeleza kuwa, madini hayo yametoka katika maeneo ya Winza Dodoma na Matombo Morogoro.4Mfanyabiashara wa Madini kutoka Kampuni ya Tom Gems Bw.Benjamin Mtalemwa akimwonesha mgeni madini mbalimbali alipotembelea banda la Tanzania. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mthamini wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Edward Rweymamu, Wa pili kulia ni Afisa Madini kutoka Shirika la Madini Tanzania (STAMICO). Bw. Peter Maha, na  wa kwanza kulia  ni Afisa toka Wizarani Bibi. Margareth Muhony.

Tupe maoni yako