Elizabeth Maxmillian
Kahama
HOSPITALI ya
serikali wilayani kahama mkoani shinyanga inakabiliwa na ukosefu wa
vitendanishi vya kupimia CD 4 kwa kipindi cha miezi miwili hali hali ambayo
imekuwa ikisababisha baadhi a wagonjwa kupoteza maisha kabla ya kutumia dawa za
kuuwa akali ya VVU.
Hayo yameelezwa jana na
mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa kahama Dr ,Deo Nyaga baada ya
madiwani kutoa malalamiko wanayoyapata toka kwa wananchi ambao
wamekuwa wakipima na kugundulika wana maambukizi ya virusivya ukimwi.
Aidha akitoa akitoa
ufafanuzi juu ya jambo hilo Dr Nyaga aliosema kuwa tatizo kubwa linaloikabili
hospitali hiyo ni ukosefu wa vitendanishi ambapo kwa sasa takribani miezi
miwili imepita ikiwa hakuna huduma ya upimaji wa CD4 inayoendelea huku
ikiwa wanategemea kupata toka bohari kuu MSD.
Hata hivyo alisema
kufuatia hali hiyo wameanza kuangalia utaratibu wa kuwaanzishia dawa wagonjwa
ambao kinga zao zitaonekana kukubalika kukabiliana na dawa hizo wakati
wakisubili uletwaji wa vitendanishi vya kupimia CD4 .
Kwa upande wao
madiwa wa halmashauri ya mji wa kahama wamemtaka mganga huyo kukaa pamoja
na watumishi wengine wa afya na kuwaeleza ukweli kutumia lugha zisizo faa kwa
wagonjwa hasa wa Ukimwi ambao kwanamna moja ama nyingine wanaweza kukatishwa
tama na kukosa matumaini kutokana na lugha za wahudumu kutokuwa nziri.
Akitoa malalamiko hayo
diwani wa kata ya mwendakulima Ntabo Majabi alisema kuwa katika utoaji wa
dawa kwa wagonjwa kuna ukiritimba unaofanywa na wahudumu wa afya katika
hospitali hiyo ya wilaya wa kuwabaguwa watu wanaowafahamu na kuwapatia dawa
huku wengine wasiojulikana wakibaki wamapenga mstari na kujikuta dawa
zikiwaishia .
Nae mwenyhekiti wa
halahsuri ya mji wa kahama Machibya Chidulamabambase aliwataka viongozi
wa kata na vijijiji kushirikiana na wataalamu wa afya kwa kuhakikisha wanatoa
elimu kwa wananchi wao juu ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU
kutokana na wagonjwa waliowengi kukata tama baada ya kukosekana kwa
vitendanishi vya kupimia CD4.
Tupe maoni yako
