IKIWA
ni takribani mwaka mmoja tangu alipoondokewa na mumewe, marehemu Juma
Kilowoko ‘Sajuki’, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema sasa yupo
tayari kuolewa lakini sharti la kwanza la muoaji lazima awe mtu mwenye
fedha zake.
Akizungumza
na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam,
Wastara alisema, amekuwa mpweke kwa muda mrefu na sasa ni wakati muafaka
wa kumpata mtu wa kuziba pengo la marehemu mume wake.
“Inatosha
sasa, nadhani muda wa kuwa na mwenzangu umefika. Napenda huyo mwanaume
awe mwenye huruma, upendo na kutambua thamani ya mke lakini ni vizuri
akiwa mwenye kujituma na awe na fedha nyingi.
“Natamani
kuolewa na bilionea. Najua nikiwa na mwanaume wa aina hiyo sitateseka,
nitapata kila ninachokitaka. Unajua mimi kama mwanamke nina mambo mengi.
Siyo siri natamani itokee siku moja niendeshe Hummer au Prado (aina za
magari) kulingana na hadhi yangu.
“Kiukweli
nitafurahi sana nikimpata mwanaume wa aina hiyo, maana nitakuwa na
uhakika wa kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kunisaidia katika
shughuli zangu za sanaa,” alisema Wastara.
Tupe maoni yako



