Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike
Shuleni hapo.
SHULE ya Sekondari ya Loyola ya Jijini
Dar es Salaam leo imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike shuleni hapo kwa
kutoa semina mbalimbali kwa wanafunzi wa kike juu ya changamoto
zinazowakabili watoto wa kike na namna ya kukabiliana nazo hasa kwa
wanafunzi shuleni.
Mada anuai zimetolewa kwa wanafunzi juu ya changamoto
zinazowakabili hasa katika kipindi hiki ambacho nchi zinazoendelea
zinakabiliwa na changamoto ya utandawazi. Miongoni mwa watoa mada
waalikwa katika maadhimisho ya siku hiyo ni Mtandao wa Jinsia Tanzania
(TGNP) ambao walitoa mada anuai kwa wanafunzi juu ya kukabiliana na
changamoto zinazowakabili hasa kipindi hiki ambacho wanahudhuria masomo
yao.
Tupe maoni yako

