banner

.

.

Tuesday, 21 January 2014

MTIHANI MWINGINE KWA KOCHA DAVID MOYES WAKATI MAN UNTED WAKIVAANA NA SUNDERLAND LEO OLD TRAFORD

MAN_U_93e2d.jpg

Timu ya Manchester United leo itaivaa timu ya Sunderland katika uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford katika mzunguko wa pili wa nusu fainali ya kombe la Capital One Cup, mshindi kati ya Manchester United au Sunderland atakumbana na Manchester City ambayo imeshafuzu hatua ya fainali itakayochezwa katika uwanja wa Wembley.

Sunderland iliutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani ''Stadium of Light'' baada ya kuitandika timu ya Manchester United magoli 2-1, hivyo timu ya Manchester United italazimika kushinda mchezo huo ili kutetea nafasi yao ya kutinga katika fainali hizo.
mechi hii itachezwa mida ya 10:45 PM kwa masaa ya afrika mashariki.
Chanzo, goal.com

Tupe maoni yako