
Timu ya Manchester City jana iliibuka
na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya West Ham United katika mzunguko wa
raundi ya pili ya kombe la ''Capita One Cup'' na hatimaye kujihakikishia
kucheza fainali ya kombe hilo itakayofanyika March 2, 2014 katika
uwanja wa Wembley, Manchester city inasubiri mshindi kati ya Manchester
united au Sunderland ambao watacheza leo katika mzunguko wa pili wa ligi
hiyo.

Alvaro Negredo aliifungia Manchester
City magoli mawili (2) wakati Sergio Arguero akimalizia goli la tatu na
kuiwezesha Manchester City kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, kwa matokeo
hayo Manchester City iliibuka na ushindi kwa jumla ya magoli 9-0 kwa
michezo yote miwili (Home and Away). Itakumbukwa kuwa Manchester City
waliibuka na ushindi wa magoli 6-0 dhidi ya West Ham United katika
uwanja wake wa nyumbani ''Etihad''
Tupe maoni yako
