Na. Magesa Jumapili (Geita)
Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhe. Magalula Saidi Magalula amewapongeza viongozi na watu
mbalimbali wote waliohusika kwa namna yeyote ile katika usimamizi wa
utekelezaji wa miradi yote ya barabara inayotekelezwa ndani ya Mkoa wa
Geita.
Mhe. Magalula
aliyasema hayo katika kikao maalum cha bodi ya ushauri ya barabara ya
Mkoa (Road Board) kilichofanyika Mjini Geita katika ukumbi wa mikutano
wa halmashauri ya Wilaya ya Geita na kuwashirikisha viongozi mbalimbali
wa Wilaya,viongozi wa vyama vya siasa na wataalam wa ujenzi wa
Katika kikao
hicho Mhe.Mkuu wa Mkoa alizitaka mamlaka za serikali za mitaa pamoja na
Tanroads Mkoa wa Geita ziendelee kuhakikisha kwamba shughuli za ujenzi
na ukarabati wa barabara zinatolewa kwa wakandarasi wenye vigezo vya
uzoefu, uwezo, wataalam na mitambo ya uhakika na pia kufuatilia na
kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kufikia kiwango
sahihi na thamani ya fedha ionekane katika miradi husika.
Katika hatua
nyingine Mhe. Magalula alizitaka Halmashauri za Wilaya kuendelea kutoa
elimu kwa wananchi kuhusu kutovamia hifadhi za barabara na pia kuweka
mipaka ya barabara ili kuepusha uharibifu wa barabara. Aidha, alitumia
nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi wenye tabia ya wizi wa alama za
barabara na kupitisha mifugo katikati ya barabara na kuacha mara moja
tabia hizo kwani zinasababisha hasara kubwa kwa serikali na kuziagiza
kamati za ulinzi na usalama,ulinzi shirikishi kuweka utaratibu mzuri wa
kulinda na kutunza barabara.
Mkoa wa Geita
una mtandao wa barabara zenye Kilometa 6,650.75 huku barabara za kiwango
cha lami zikiwa ni kilometa 485, changarawe ni kilometa 3,381.05 na
barabara za udongo ni kilometa 2,784.70.
Miradi
inayotekelezwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na ujenzi wa barabara ya
“Round about” – Benki ya CRDB – Hospitali ya Wilaya – Benki ya NMB na
kuunga barabara kuu ( KM 1) kwa usimamizi wa Tanroads kwa gharama ya
Tshs 450 milioni imekamilika kwa asilimia 98.Ujenzi wa barabara ya
Nyankumbu-Nyanghwale (km 91) unaendelea kujengwa kwa KM 2 kutoka
Nyankumbu hadi Mkolani ujenzi umefikia asilimia 60 na itagharimu kiasi
cha million 750 mpaka kukamilisha kilometa 2 za lami ujenzi huo
unasimamiwa na Tanroads. Aidha kuna ujenzi unaoendelea wa barabara ya
CRDB- Boman i- Magereza (km1) kwa kiwango cha lami ambao umefikia
asilimia 24 ambao utagharimu Tshs 438 milioni.
Miradi mikubwa
ya ujenzi wa barabara inayotekelezwa na serikali na kusimamiwa na
Tanroads katika Mkoa wa Geita ni pamoja na Bwanga- Biharamulo (KM 67)
kwa gharama ya Tshs 55 bilioni na Bwanga –Uyovu (KM 45) kwa gharama ya
Tshs 43.3 bilioni miradi hii yote imefikia asilimia nzuri na iliwekewa
jiwe la msingi na Mhe. Rais wakati wa ziara yake Mkoani Geita.
Tupe maoni yako

