
Na Magreth Kinabo – Maelezo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
amewataka Watanzania kuongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya Virusi Vya
Ukimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili katika Tanzania iweze
kuwa na kizazi kisichokuwa na VVU na ugonjwa wa Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau wa kuzuia maambukizi
ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha mama Kikwete aliwataka
Watanzania kuchangia sh. 100 katika kupambana na tatizo kwa mchango
utawapa nguvu wadau wengine kuwaunga mkono.
Aliwataka wadau wamaendeleo kuendele kuunga mkno katika juhudi za kuondokana na tatizo hilo.
" Lazima juhudi za makusudi zifanyike
bila kuchoka kwa maeneo yote Serikali, NGO's, taasisi za dini mashirika
ya kiraia na watu binafsi . Hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na kuwa
na nguvu kazi iliyobora, kizazi kisichokuwa na maambukizi na VVU na
Ukimwi," alisema Mama Kikwete huku akisisitiza Tanzania bila Ukimwi
inawezekana.
Aliongeza kuwa mikakati imara na
endelevu ni lazima iwepo kama vile kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya
VVU na Ukimwi kwa kushirikisha jamii na kutoa tiba kikamilifu zinaweza
kupunguza maambukizi hayo
Tupe maoni yako
