
JAMBO ambalo linaiumiza kichwa Yanga
sasa ni kutaka kuhakiki kama kweli Etoile du Sahel imewasilisha jina la
straika, Emmanuel Okwi kwenye usajili wake kwa Shirikisho la Soka Afrika
(CAF).
Lakini katika orodha ya Etoile du
Sahel, ambayo Mwanaspoti imepata nakala yake jana Ijumaa ni kwamba
klabu
hiyo imepeleka CAF majina 24 tu, na hakuna jina la Emmanuel Okwi.
Iwapo ikitinga hatua ya makundi ya
Ligi ya Mabingwa Afrika, Etoile inaweza kuongeza majina sita kwani kila
klabu inaruhusiwa kutuma majina 30.
Kwa kifupi ni kwamba, Etoile du Sahel
haiwezi kumtumia Okwi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa Yanga
wanaweza kumtumia raia huyo wa Uganda kwani wametuma jina lake katika
shirikisho hilo mjini Cairo, Misri.
Etoile kwenye usajili wake wa CAF imepeleka wachezaji 24 ambao pia hakuna jina la Okwi.
Waliosajiliwa CAF ni Aymen Mathlouthi,
Saif Ghezal, Ghazi Abderrazzak, Radhouene Felhi, Marouene Tej, Hamza
Lahmar, Alaya Brigui, Baghdad Bounedjah, Abdel Fadel Suanon, Issam
Jebali, Franck Kom, Ahmed Mortadha na Ben Ouannes
Tupe maoni yako
