Hapa ni Meneja wa kituo hicho Marium Juma,akitoa maelezo juu ya Tuzo..
Wafanya kazi wa kwaneema Fm,wakifuatilia tukio zima.
Frola Jackson,ambae amechukua tuzo ya mfanya kazi bora wa usafi wa 98.2.
Mkurugezi Dinnah Mpemba katika Pozi safiiiiiiiiiiiiii sanaaaaaaaaaaaaa..........
Joshua Dede,akichekelea baada ya kupokea Tuzo............
Erasto Juma akionesha cheti cha mbunifu bora katika kipindi cha kijana
Ilikuwa ni Furaha na nderemo isiyo kifani....
Afisa Utawala Msaidizi ambaye pia ni Meneja Vipindi wa Kwaneema Fm Jackline Raphaely akionyesha cheti cha Mfanyakazi bora 2013 alichokipata leo baada ya kuibuka msomaji wa taarifa ya habari bora.
| Mzee wa Habariiiiiiiiiiiii, Chief Editor Jeston Kihwelu akipokea barua ya utambuzi kwa kazi yake. |
Erasto Juma na Joshua Dede wakiwa na Mkurugenzi wa Kwaneema Fm Dinnah Mpemba.
Picha ya jopo la Wafanyakazi na Watangazaji wa Kwaneema fm.
Washindi wa tuzo mbalimbali upande wa wanawake wakionekana mbele ya ofisi ya Kwaneema fm.
Mshindi wa Tuzo ya Mfanyakazi bora 2013 Jackline Raphaely akiongea juu ya tuzo aliyopata kutoka kituo cha Redio Kwaneema fm.
Jacktan Msafiri akiongea na Erasto Juma.
Mwandishi wa habari wa Kwaneema Fm Jacktan Msafiri akiongea na Joel Maduka juu ya tuzo aliyopata.
Mmiliki wa Matukio Media Blog Fabian Fanuel akiwa na Mtangazaji wa Kwaneema Fm Joel Maduka.
Mhariri Mkuu wa Kwaneeema Fm Bw.Jeston Kiwelu na Maneja Msaidizi Mariam Juma wakishow mbele ya Kamera ya Matukio Media Blog.
Joel Maduka
Mwanza.
Imebainika kuwa kufanya kazi kwa wito pasipo kuweka
Maslahi mbele ni silaha ya kushinda hali ngumu ya maisha.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa kituo cha radio ya
kwaneema Pastor Dinnar Mpemba katika hafla za kutunuku tuzo kwa wafanyakazi
bora katika Mwaka wa 2013
Akiwataja washindi wa tuzo mbalimbali Meneja wa
Kituo hicho Mariam Juma amewapongeza na kuwataka wazidishe bidii katika kazi na kuzidisha ubunifu mwaka huu.
Kwa upande wao baadhi washindi wa tuzo hizo Joel
Maduka, Spencioza Haule, Frola John wameelezea hisia zao baada ya kupata tuzo
na kuahidi kujituma zaidi kwa mwaka huu mpya ambao anaanza.
Naye Meneja wa vipindi katika kituo hicho Jackline
Raphael ambaye ndiye Mshindi wa tuzo ya Mfanyakazi bora ameeleza Siri ya Ushindi
wake kuwa ni Mungu na pia kujituma sana katika kazi bila kijihurumia.
Tuzo zilizotolewa ni katika ngazi ya Mfanyakazi bora
wa Mwaka mbunifu,Mfanya shughuli kwa kujituma,Mfanyakazi anayejitolea katika
kazi ka ziada Mtunza muda na aliyefanya vizuri katika kuleta wageni katika vipindi.
Tupe maoni yako
