Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man, amesema mpenzi wake wa
kwanza katika maisha yake ni mwanadada muigizaji wa filamu nchini Rose
Ndauka,ambaye waliachana tangu 2006.
Akizungumza
na XXL ya Clouds Fm leo Tunda amesema walikuwa wakikutana na mwanadada
huyo katika studio moja huko kariakoo hali iliyowapelekea kuanza
mahusiano yao yamapenzi.
“Kuna studio moja kariakoo,wanadada walikuwa wanakuja kuchana na yeye
anakuja studio anaangalia situation zinavyoenda, kwahiyo kuanzia hapo
ndiyo akaanza kunijua nini, nikaenda kwao kila kitu kikawa fresh
kila kitu kikawa kinaenda poa ni 2006 kitu kama hicho, yani tumeachana
kabla, hamna hata mmoja aliyekuwa star, sasa tumejikuta kila mmoja
anafanya issue zake na mimi nafanya issue zangu, mpaka sasa hivi
nikikutana nae, nasikia ameolewa peace tu ,kama na shida na yeye
kwasababu na yeye sasa hivi anapiga mapigo ya movie na mimi na movie
zangu kama vipi namdondosha halafu namlipa”, alisema Tunda.
Tupe maoni yako

