Mwenyekiti Wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu TFF, Rahim Shaaban akizungumza na wanahabari amesema kwamba migogoro iliyokuwa ikiendelea kati ya mwenyekiti wa nidhamu ndiyo iliyopelekea adhabu Wakili Ndumbaro kufungiwa kujihusisha na soka.
Bwana Shaaban amesema wamepitia mashauri hayo na kugundua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu Jarome Msemwa ilikua na mgogoro kwa kuwa hakukuwa na busara iliyotumika katika utoaji wa adhabu kwani tarehe ambayo Ndumbalo aliyoitwa na kamati ya Bw. Jarome tayari alishaomba ruhusa ya safari na siku iliyotoka hukumu ndiyo siku aliyokuwa safarini.
Ndumbaro ambaye ameshatumikia kifungo cha miaka miwili na miezi tisa aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Malinzi baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, .
Inaaminika kwamba Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.
Kikao cha cha kamati ya nidhamu kilifikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu, alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi ambayo baadae alimkana hadharani kwa madai alitamka kwa utashi wake
Tupe maoni yako

