banner

.

.

Saturday 22 July 2017

SINGIDA UNITED YAIBOMOA YANGA

Klabu ya Singida United ambayo imepanda daraja na kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu imemaliza usajili wake kwa kuibomoa klabu ya Yanga baada ya kumsajili aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke. 






Aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi na kocha wa zamani wa Yanga , Hans Pluijm ambaye sasa ni kocha mkuu wa klabu ya Singida United alisema kuwa katika klabu yake hiyo alikuwa amebakiwa na nafasi moja ili kujenga kikosi chake vizuri, nafasi hiyo ambayo imejazwa na Kaseke. 
Mkurugenzi wa Singida United Bw. Festo R. Sanga amethibitisha kuchukuliwa kwa Deus Kaseke katika klabu yake hiyo na kusema amesaini mkataba wa miaka miwili.
"Hatimaye Deus David Kaseke anaswa na Singida United, amesaini kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia timu yetu na tayari anaelekea Mwanza kuungana na wenzake" alisema Festo Sanga

Timu ya Singida United itakutana na klabu ya Yanga katika mchezo wa kirafiki ambao utafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 5/08/2017 uwanja wa Taifa.

Tupe maoni yako