Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhutubia Bunge Maalum Machi 21 mwaka huu mjini DodomaKauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa ofisi za Bunge mjini Dodoma.
"Kwa mujibu wa kanuni ya 75 (1), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge Maalum siku ya Ijumaa Machi 21 ,mwaka 2014 saa 10:jioni, ambapo wageni waalikwa wote watatakiwa kuwa wameingia na kuketi katika maeneo watakayoelekezwa saa 9:00 alasiri," alisema Katibu huyo.
Aidha Katibu huyo alisema ratiba ya shughuli hiyo itaanza na kikao cha Bunge saa 9:10 na baadae kikao hicho kitaanza saa 9:20 kwa ajili ya kumpokea Rais.
Tupe maoni yako

