Joel Maduka
Mwanza
UCHUNGUZI wa saratani ya mlango wa kizazi na
saratani ya matiti umezinduliwa leo mkoani mwanza kwa katika kuadhimisha siku
ya mwanamke duniani.
Akizindua uchunguzi huo Mwenyekiti wa Wama Mama Salma Kikwete,amesema
kuwa ni vyema kwa wadau wa maendeleo, kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa
wanawake kwani unapo muelemisha mwanamke
mmoja ni sawa umeelimisha watu wengi katika jamii.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Dk,Deonard
Mbando,amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo imekuwa na kiwango kikubwa kwa
tatizo la saratani ya kizazi.
Aidha Mwenyekiti wa Madaktari Wanawake Tanzania,Dk Serafina
Mkuwa,ameongeza kuwa saratani ya mlango
wa kizazi ndio inaongoza kwa kuwapata wanawake wengi na kusababisha vifo vingi
hasa katika nchi zetu za kiafrika ikiwemo Tanzania.
Uzinduzi wa saratani ya kizazi na saratani ya matiti
umezinduliwa leo katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza,huki ikiwa imebeba
kauli mbiu isemayo tuungane pamoja katika kutokomeza saratani ya mlango wa kizazi Tanzania, nani
kama Mama.
Tupe maoni yako