banner

.

.

Tuesday, 25 February 2014

NCHI YA TANZANIA YASISITIZA NYONGEZA YA POSHO KWA WALINZI WA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA.



Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  imesema, posho ya dola 1.28  kwa siku wanayolipwa walinzi wa amani wanaohudumu katika Misheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa,  hailingani na  mazingira magumu  na hatari ya utekelezaji wa mamlaka wanayokabidhiwa na Umoja wa Mataifa. 
        Na kwa sababu hiyo ,na kwa zingatia hali halisi,  Tanzania  imesisiza kwamba,  wakati umefika sasa wa kuangalia upya posho hiyo ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 20.
       Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania katika Umoja wa mataifa,  ametoa rai hiyo  mwanzo mwa  mkutano wa Kamati   Maalum  ya      Usimamizi wa  Operesheni za Ulinzi wa    Amani maarufu kama C-34.
       Kamati hii ambayo wajumbe wake ni kutoka nchi zinazochangia walinzi wa Amani katika misheni mbalimbali za kulinda  amani,  imeanza mkutano wake wa  mwezi mmoja hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo  wajumbe watajadili  mambo yote yanayohusu sera za ulinzi wa Amani  chini ya Umoja wa Mataifa.
       Balozi Manongi amewaeleza wajumbe wa mkutano huo  kwamba   Kamati   ilikuwa inaanza mkutano wake,  wakati ambapo ,  operesheni za ulinzi wa amani  zinakabiliwa na  changamoto mbalimbali zikiwamo za malipo duni.

Tupe maoni yako