banner

.

.

Monday 24 February 2014

MAN UNITED USO KWA USO NA OLYMPIAKOS KATIKA KLABU BINGWA ULAYA LEO



UNITED_718df.jpg
Manchester United wataingia dimbani bila walinzi wake wawili; Phil Jones na Jonny Evans katika mchezo wao wa hatua ya kwanza wa ligi kuu ya mabingwa ulaya uatakaochezwa usiku wa leo, tarehe 25/02/2014, walinzi hao wapo majeruhi.
Mashetani hao wekundu pia watamkosa mshambuliaji wake mahiri Luis Nani ambae nae ni majeruhi wakati Rafael na Danny Welbeck wote wakitokea majeruhi watajiunga na kikosi cha timu hiyo tayari kupambana na mabingwa wa kigiriki, timu ya Olympiakos.
Olympiakos pia itamkosa mpachika nyavu wao ''Javier Saviola ambaye yupo majeruhi. Hivyo safu ya ushambuliaji wa timu hiyo itaongozwa na raia wa Nigeria, Michael Olaitan (21).
Japokuwa hali bado ndivyo sivyo kwa timu ya Olympiakos kwani Nelson Valdez aliyesajiliwa msimu wa Januari haileweki kama atakuwa tayari kucheza au la; lakini kocha wa timu hiyo ''Michael'' alisema mchezaji huyo yupo lakini hakuelezea kama atampanga au kutompanga alipokuwa ulizwa kuhusu uimara wa mchezaji huyo mwenye asili ya nchi ya ''Paraguay''.
Mabingwa hao wakigiriki watakutana na mabingwa kutoka uingereza, timu ya Manchester United katika uwanja wa Karaiskakis Stadium, Athens, leo usiku hivyo Man United watakuwa ugenini wakati safu ya ushambuliaji wao itaongozwa na washambuliaji mahiri kama Wayne Rooney na Rob Van Persie.
Michezo itakayochezwa leo usiku katika klabu bingwa ulaya
UNITED_2_62516.png

Tupe maoni yako