Picha ya pamoja
MAAFISA Afya na Mifugo wametakiwa kutobweteka maofisini na kufanyia kazi kwenye makaratasi(Paper Work) badala yake watumie taaluma yao kama walivyofundishwa mashuleni kwa kufanya kazi ya vitendo.
Mwito huo umetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Agnes Buchwa, alipokuwa akifungua kikao cha watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya kuhusu Shughuli za Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba(TFDA) kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya uliopo Forest Mpya Jijini hapa.
|