banner

.

.

Thursday, 30 January 2014

WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII MHE. LAZARO NYALANDU AWAAGIZA WAVAMIZI KUONDOKA NCHINI MARA MOJA..

nyalandu_eb397.png

Na mwandishi wetu mwananchi
 Tabora. Serikali imesema haitaogopa wala kumvumilia mtu atakayevamia maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba kwa lengo la kuhujumu maliasili.

Hali kadhalika kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika maeneo hayo.
Pia, imewataka watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi kuondoka kwa hiyari yao badala ya kusubiri kuondolewa kwa nguvu.

Hayo yalisemwa juzi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipokuwa akizungumza na maofisa na watumishi wa Idara ya Wanyamapori katika Kanda ya Magharibi.

Agizo hilo limetokana na taarifa za kuvamiwa kwa baadhi ya maeneo ya Hifadhi za Pori la Akiba la Ugalla na Moyowosi, ambapo baadhi ya wafugaji wameingiza mifugo huku baadhi wakijihusisha na ujangili.
Maofisa wa wanyamapori walisema wafugaji hao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuingia na silaha kwenye hifadhi na kuwinda wanyama wakiwemo tembo na mamba.
chanzo: Mwananchi.

Tupe maoni yako