Kahama.
IMEELEZWA kuwa uwepo wa
mila na desturi potofu ikiwemo tamaa ya kupata mali ni sababu
inayopelekea wazazi kushindwa kuzungumza na watoto wao juu ya afya ya
uzazi hali inayosababisha kuwepo kwa ndoa na mimba za utotoni
Hayo yalibainishwa na baadhi ya wasichana wa kata ya Shilela wilayani kahama mkoani shinyanga katika mahojiano na mwandishi wa habari hii ambapo walisema katika jamii nyingi za kisukuma wazazi hawana desturi za kuzungumza na watoto wao hasa katika masuala ya afya ya uzazi.
Mmoja wa wasichna hao Semeni Maziku alisema kuwa wazazi wengi huwalazimisha watoto wao wa kike kuolewa mara tu wanapohitimu elimu ya msingi na baadhi yao kuwashinikiza kufanya vibaya katika mitihai ili washindwe kuendelea na masomo na badala yake waolewe.
Aidha maziku kwa upande wake alisema tayari yeye aliolewa akiwa na umri wa miaka 14 ambapo alikaa kwa muda wa mwaka mmoja ndani ya ndoa yake na baadae alitoroka kutokana na ugumu wa maisha huku akiacha mtoto mmoja kwa mwanaume alikuwa amemuoa.
Kufuatia hali hiyo ya kuongezaka kwa ndoa na mimba za utotoni shirika lisilokuwa la kiserikali la Kiota Women Health Development [KIWOHEDE] la jijini Dar es salaam limeanzisha mradi wa kuwapatia elimu ya afya ya uzazi wasichana waliokatisha masomo yao na kupata ujauzito kwa lengola kupunguza tatizo hilo.
Mkurugenzi wa shirika hilo Justa Mwaituka alisema kuwa katika mradi huo unaoendeshwa kwenye kata nne za Lunguya,Shilela, Busoka na Mhongolo wilayani humo utalenga wasichana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 ambao watapatiwa elimu hiyo pamoja na elimu ya ufundi stadi na wengine watarejeshwa mashuleni kadri watakavyo hitaji.
Hata hivyo Mwaituka alisema lengo la mradi kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 ni kufikia wasichana 350 ambapo zaidi wa wasichana 700 wamejitokeza katika kujiunga na mradi huo na 24 wamepelekwa kupata mafuno ya ufundi stadi ya ushonaji chelehani huku waliobaki wametengea vituo vya kujifunzia katika maeneoyao yatakayoendeshwa na shirika hilo.
Mwaituka alitoa wito kwa serikali kushirikiana na mashirika katika kutoomeza wimbi la mimba na ndoa za utotoni kwa kuhakikisha inaweka mipango madhubuti itakayomfanya mtoto wa kike anapata elimu na kutimizamalengo yake .
Tupe maoni yako
