banner

.

.

Wednesday 29 January 2014

NITAHAKIKISHA SANAA YA UIGIZAJI MWANZA INASIMAMA NA KUPENDWA NA WADAU WOTE.

Msanii Masele Malekela.
Msanii Mkali wa Sanaa ya uigizaji kutoka Rocky City Mwanza Masele Malekela amesema kuwa atahakikisha sanaa ya uigizaji Mwanza inasimama na kupendwa na wadau wa sanaa uigizaji almaarufu  Filamu kwa sababu umechoka na sanaa ya Mwanza kuonekana  si kitu.

Akizungumza na mtandao wa www.matukiomedia,blogspot.com Msanii Masele amesema kuwa muda umefika kwa wadau na wapenzi wa filamu kuondoa fikra potovu kwamba wasanii wa Mwanza hawawezi kuigiza muvi nzuri.

Mtandao wa www.matukiomedia.blogspot ilimtafuta Msanii Masele ili kuzungumza nae.

Matukio Media Blog: Kwanini Watu hawapendi sanaa ya Mwanza?
Masele: Sio kwamba watu hawapendi sanaa,  tatizo la kwanza wasanii wa Mwanza wa hawajitambui kuwa sanaa ya uigizaji ni kazi kama kazi nyingine, hivyo kutoipa nafasi ya kwanza.

Matukio Media Blog: Baada ya kugundua tatizo hilo, umepanga kufanya nini ili kuliondoa?
Masele: Bado najipanga pindi nitakapokuwa na muda nitakuwa na semina na wasanii wote wa Mwanza kwa kusudi la kutoa Elimu ya kujitambua kuwa wao ni nani na wanapaswa kufanya nini ili kuinua sanaa ya Mwanza.

Matukio Media Blog: Ukiangalia baadhi ya kazi za sanaa za Mwanza zinakosa ubora unaotakiwa katika uigizaji, wewe kama Msanii unahisi tatizo liko wapi?
Masele: Tatizo liko kwa waongozaji filamu maana Msanii, Kamera man , Edita wote wanapokea maelekezo kutoka kwa Waongozaji wa filamu{ Madirector}, hivyo basi madirector wa Mwanza wanatakiwa wajipange kufanya kazi ya ubora.

Matukio Meda Blog: Zipi changamoto mnazokutana nazo katika tasnia ya uigizaji?
Masele:   a.Uchanga wa Soko la Filamu Mwanza
             b. Maeneo ya kushutia 
             c. Uelewa mdogo wa Baadhi ya Watu kuamini kwamba kila anayefanya sanaa ni malaya.
             d. Sapoti kuwa ndogo kutoka kwa wadhamini.
             e. Baadhi ya waongozaji wa filamu kuwa na tabia mbaya ya kuwataka kimapenzi wasanii wa kike.

Matukio Media Blog: Kama msanii na mwaharakati wa kukomboa sanaa ya Mwanza ipendwe, una lipi la mwisho la kuwaambia wasanii, wadau na wote wenye mapenzi mema na sanaa ya Tanzania?
Masele: Wasanii wajitambue na wajue nini wanafanya, wasifanye sanaa kama sehemu ya kupotezea muda, kwa wadau na wote wenye mapenzi na sanaa, watoe sapoti kwa wasanii pindi wanapotoa kazi zao za sanaa yaani Muvi na kuwapa sehemu za kushutia ili kuwawezesha kufanya kazi za kiwango zaidi.



Tupe maoni yako