banner

.

.

Friday 31 January 2014

MATUKIO NA PICHA KATIKA MKESHA NDANI YA JB BELMONT MWANZA

Mr Shigongo wa kwanza kushoto akiwa na Mark msemo wakiimba wakimsindikiza mwimbaji Ajuaye Onesmo wakati akiimba katika mkesha uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Jb Belmont  Mwanza
Moja katika ya staili ya ukweli ambao vijana hao waliitupia katika steji wakati mambo matamu yakiendelea..
Mwimbaji Betty Lucas Mama wa Unaona nini akiimba kwa hisia katik kesha wa Ijumaa katika ukumbi wa Hotel ya Jb Belmont Mwanza.
Mwimbaji Onesmo Ajuaye akiwajibika kwa steji wakati wa fursa ya kuimba katika mkesha wa ajabu wa Nguvu za Mungu uliofanyika usiku wa kuamkia jana Ijumaa.
Umati wa watu waliofika katika mkesha huu wakisikiliza neno la Mungu lililokuwa likifundishwa na Mchungaji Dr Michael Kulola.
Watu wakisiliza maelekezo kutoka kwa Mchungaji Michale Kulola amabye haonekani pichani.
                   Wakati wa kuadudu ukiendelea katika ukumbi wa Jb Belmont.
Watoto wa mjini City Centre Choir wakiimba wimbo mtamu sana ambao nadhani kwako hujawai kuusikia unaoitwa Mungu ni Mwaminifu. Leo Jumamosi utapata fursa ya kuusikia katika kipindi cha Ngurumo za Waimbaji kupitia kituo cha redio cha Kwaneema Fm 98.2 kama uko Mwanza na Kanda ya Ziwa kuanzia saa 6-8 mchana.
        Wakati wa sifa ni kusifu kweli kila mtu kwa staili yake kama inavyoonekana pichani.
Soloist wa kimataifa ambae pia mama Pastor Michael Kulola akiwaongoza wainakwaya wa City Centre wakati wakimba katika mkesha wa Ijumaa katika ukumbi wa Jb Belmont. Kiwango alichokionyesha hakijawai kuonekana toka aanze kuimba kwaya.

Tupe maoni yako