banner

.

.

Monday, 27 January 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA JIJINI MWANZA.

Na Peter Fabian 

MWANZA. 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mbaraka Abduwakili amewataka wajumbe wa Baraza kuu la Taifa  Idara ya Uhamiaji nchini kujikita zaidi kujadili utendaji kazi wa watumishi wa Idara hiyo.

Kufanya thathimini ya utendaji wa watumishi ambao baadhi yao wamekaa muda mrefu kwenye vituo vyao vya kazi  na kuzoeana hali ambayo imedaiwa na kudhaniwa kuwa inazorotesha ufanisi wa majukumu ya kila siku na hata huduma kutolewa kwa wageni na wananchi bila kukidhi ubora wa maadili ya viapo vya kazi.
Akifungua Mkutano mkuu wa Baraza hilo jana Jijini Mwanza , alisema kwamba baadhi ya askari na watumishi wa Wizara yake wanadaiwa kukaa muda mrefu sehemu moja ikiwa ni kwenye vituyo vyao vya kazi jambo ambalo linachangia baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na kujihusisha na ulevi na vitendo ambavyo haviruhusiwi na kuzorotesha ufanisi wakati wa utowaji huduma.
Abduwakili alisema kwamba mazoea ya watumishi hao wa Idara zilizo chini ya Wizara yake ni vyema wakazingatia viapo vya utendaji wao wa kazi na kujikita kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kwani hata solidalite yao inasema kwamba masilai bora kwanza lakini pia utendaji bora wa kazi.
Abduwakili aliwataka wajumbe 130 ambao ni wawakirishi wa watumishi na viongozi wa vyama vya wafanyakazi katika Idara  za Uhamiaji kutoka Mikoa yote nchini kuzingatia kujadili uboreshwaji wa utendaji kazi zaidi pamoja na kuweka mapendekezo ya kuboreshewa masilahi yao lakini wawafikishie ujumbe wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwenye vituo vyao vya kazi.

Tupe maoni yako