![]() |
| Afisa habari wa Taasisi ya Sayansi Jamii (TASAJA) Bituro Kazeri akizungumzia sakata hilo mbele ya waandishi wa habari leo. |
TAASISI ya Sayansi
Jamii (TASAJA) mgomo si njia ya kumaliza tatizo la mashine za kutolea
Ankala za (EFD) zinazotakiwa kuanza kutumika kuanzia January Mosi kwa
utaratibu uliowekwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
unaoendelea toka jana Jijini Mwanza.
Akizungumza na vyombo vya
Habari leo Jijini hapa, Afisa habari wa Taasisi hiyo Bituro Kazeri
alisema kwamba kufatia mgomo baridi unaoendelea wa wafanyabiashara wa
maduka makubwa ya kati na rejareja kupinga kupatiwa mashine za kutolea
ankala za mauzo ya bidhaa wanazouza kwa wateja kwa madai kuwa bei yake
ni kubwa kuliko uwezo wa wawafanyabiashara hao jambo limeleta sitofahamu
kwa wananchi.
Kazeri ameeleza kuwa kutokana na mgomo huo kuingia siku ya pili leo,
taasisi hiyo imekugwa na imeamua kutoa tamko lake, taasisi hii ambayo
imeanzishwa na Wahitimu wa Vyuo vikuu nchini waliosoma Elimu ya Sayansi
Jamii ambayo inajihusisha na masuala yanayohusu jamii, hivyo kuguswa na
kuchukua hatua za kuitaka serikali na wafanyabiashara hao kuketi meza
moja kwa mazungumzo ili kurejesha huduma kwa wananchi.
“Wafanyabiashara ni sehemu ya jamii na muhimu kwa usitawi wa nchi yetu,
kuendelea kuwepo kwa mgomo huo unaosababishwa na kundi mojawapo ikiwa ni
wafanyabiashara, serikali na chombo cha kukusanya Kodi kunaweza
kukaathili jamii kwa kiwango kikubwa kupata huduma na mahitaji mhimu, ni
vyema kukatumika taratibu na malidhiano yatakayomaliza mgomo huo kwa
njia ya mazungumzo kwenye meza” alisema.
Afisa habari huyo alisema, Taasisi hiyo muhimu ya masuala ya jamii
inaona ni vyema sasa Serikali ikatoa Elimu kwanza pili ikakubali
kuchukua mzigo wa kugharamia mashine hizo kupitia mashirika ya fedha ya
kimataifa kupata mikopo ikiwemo Benki ya Dunia na mashirika mengine
yanayojihusisha na masuala ya fedha ili serikali iweze kuzitoa mashine
hizo kwa wafanyabiashara kwa gharama nafuu zaidi ambazo zitarejeshwa
kidogokidogo hadi kumaliza deni.
“ Mfano mzuri TRA itoe mshine hizo za EFD kwa wafanyabiashara kama
Makampuni ya kutengeneza vinywaji baridi ya Coca Cola, PEPSI, TBL na SBL
ambayo yanawagawia wateja wake Friji na kuwataka kununua bidhaa za
Makampuni hayo kwa taratibu na mikataba waliyokubaliana, jambo ambalo
hili likifanya na TRA kuwapatia wafanyabiashara hao kwa bei ndogo zaidi
basi wanaweza kurudisha garama hizo kidogo wakati wa kupeleka mapato ya
kila mwezi” alieleza.
![]() |
| Eneo la maduka pembezoni mwa Salmacone Mwanza. |
Taasisi hiyo inatoa wito
kwa wafanyabiashara wasiokuwa na tatizo la mashine hizo kuendelea kutoa
huduma kwa wananchi na kwani TRA imekwisha warudishi fedha zao
walizokwisha toa kulipia mashine hizo za Ankala na kuwataka
wafanyabiashara wanaopinga kutumia wakae meza ya mazungumzo na viongozi
wa Serikali, TRA na wadau wengine kumaliza tatizo lililopo badala ya
kuzuia huduma kwa wengine kuendelea kutoa.
“Mgomo huu usiingiliwe na
wanasiasa na baadhi ya kundi la watu wachache wanaotaka kutumia kivuli
cha mashine za EFD kutekeleza majukumu yao kwa kisingizio cha
kuhamasisha mgomo huku wanapotakiwa kukaa kwa pamoja kwa ajili ya
mazungumzo kukataa na kuanza kutoa mashariti ya siyiyokuwa na hata
chembe ya tija huku pia wakitoa vitisho vya kuchoma moto” alisema
Kazeri.
Aliongeza kuwa ni uoga tu
uliopo juu ya utumiaji wa mashine hizo lakini kimsingi teknolojia hii
ya mashine ambayo hutumika duniani kote kukusanya Kodi na itawezesha na
kurahishia TRA kukadilia mapato kwa mfanyabiashara atakayekuwa yuko
registard kutumia mashine hizo na itaondoa ukwepaji wa kodi na siyo
dhuma na unyonyaji wa mapato hivyo ni vyema ikaondolewa hofu hiyo na kwa
Sayansi ya Teknolojia na hoja ya wafanyabiasha kimsingi ni nzuri lakini
mwisho wa yote ni lazima kulipa mapato.
Ameitaka serikali pia
kuwa makini na watu ambao wamekuwa wakijipa vyeo vya kuongoza makundi ya
kijamii na kutoa matamko mbalimbali kwa kuwatambua na kujua uhalali wao
katika makundi wanayowawakilisha ili kudhibiti nchi hii kuwa na watu
wanaojiamlia na kufanya mambo yasiolitakia mema taifa letu na wananchi
kwa ujumla kwa kuchukua hatua na kutumia sheria zilizopo.
![]() |
| Maduka ya mitaa yote ya mitaa muhimu katikati ya jijini Mwanza yamepigwa kufuli na wamiliki wake kujipa mapumziko ya muda usiojulikana kutokana na mgomo unaoendelea. |
![]() |
| Kuelekea Pangani Music Centre. |
![]() |
| Kwa Mukpar. |
![]() |
| Ofisi za huduma za utalii. |
![]() |
| Barabara ya Nyerere. |
![]() |
| Food Square na jengo la Toto. |
![]() |
| Kuelekea Delux Night Club. |
Tupe maoni yako










