London, England. LIVERPOOL imeiambia PSG italazimika kutoa Pauni 87 milioni kama inataka kumnasa kiungo, Philippe Coutinho.
PSG imeulizia kuhusu upatikanaji wa Coutinho na hilo ndilo jibu ambalo imepewa wakati huu Liverpool ikionekana kutokuwa na dhamira ya kumuuza staa huyo ambaye pia amekuwa akinyemelewa na Barcelona.
Katika hatua nyingine Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anataka viongozi wa klabu yake kuhakikisha wanafanya mazungumzo na klabu ya RB Leipzig kuangalia uwezekano wa kumchukua kiungo wao mahiri, Naby Keita ambaye anamtamani kwa muda mrefu.
Klabu hiyo ya Ujerumani inataka Pauni 80 milioni kwa ajili ya staa huyo wa kimataifa wa Guinea lakini pia imekuwa na ugumu wa kumuuza kwa sababu msimu ujao itashiriki katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza.
Tupe maoni yako