BEKI wa kati wa Simba, Abdi Banda, juzi Jumapili jioni alisaini mkataba wa miaka mitatu katika klabu ya Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini na yupo kwenye kambi ya Taifa Stars iliyoko kwenye michuano ya Cosafa.
Taarifa ambazo hazina shaka kuwa beki huyo amekula mkataba mnono Baroka na yeye mwenyewe aliweka jina la timu hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Kuna timu imenipa mkataba nimefikia makubaliano ya kila kitu na kinachosubiriwa ni mimi kusaini mkataba tu,” alisema Banda ambaye yupo katika mashindano ya Cosafa na kikosi cha Taifa Stars ambacho kimetinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Boniface Pawasa, alisema kuwa kuondoka kwa Banda ni pigo kubwa sana katika safu ya ulinzi ya Simba na viongozi wanatakiwa kuangalia kwa jicho la mbali zaidi kumtafuta beki sahihi wa kuziba nafasi hiyo.
“Licha ya kuwa na makosa ya utovu wa nidhamu alikuwa mmoja wa beki sahihi wa kati wa Simba, lakini pia alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja kwa hiyo kukosekana kwake Simba wanatakiwa kumtafuta mbadala wake, lakini pia natoa pongezi kwa maamuzi aliyoyafanya,”alisisitiza.
“Katika maisha ya soka hayo ndio maamuzi sahihi kwa mchezaji anayesaka maendeleo.” Naili uweze kufanikiwa katika mchezo wa mpira wa miguu nilazima uwe na maamuzi sahihi yatakayo kufanya kupiga hatua katika maisha ya mpira.
Tupe maoni yako