Klabu ya Manchester United imeandaa Pauni 40 milioni kwa ajii ya kuipata saini ya kiungo Radja Nainggolan na kocha Jose Mourinho tayari alishaeleza nia yake ya kumtumia mchezaji huyo msimu ujao.
Nainggolan ameitumikia Roma misimu mitatu na nusu tangu alipohamia akitokea Cagliari mwaka 2014. Hata hivyo, inaelezwa alikataa ofa kutoka Chelsea msimu wa kiangazi uliopita yenye thamani hiyohiyo.
Mchezaji huyo mwenye maiaka 29 thamani yake inaonekana kushuka kutokana na umri, pia klabu yake ipo tayari kumuachia ili kukijenga upya kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.
Taarifa zinaeleza kuwa Manchester United imejipanga kumpa mshahara wa Pauni 125,000 kwa wiki na mazungumzo ya awali tayali yamemalizika kati ya timu ya Machester Untd pamoja na timu ya Fc Roma ya Mjini Italia, hata hivyo mchezaji huyo amekiri kutokuwa na furaha katika klabu yake hivyo itakuwa rahisi kwa klabu ya machester Untd kuipata saini ya mchezaji huyo.
Tupe maoni yako