Joel Maduka
Mwanza
Wakazi wa Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa wameombwa
kujitokeza kushuhudia tamasha kubwa la Muziki wa Injili linalojulikana kama
Pasaka Gospel Festival 2014 ambalo linaandaliwa na Kampuni ya The Great Zone
Entertainment katika Sikukuu ya Pasaka Mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba
Mwanza .
Haya yamesemwa na Mratibu wa Tamasha hilo bwana Fabian Fanuel wakati akizungumza na waandishi
wa habari wakati akizungumzia ujio mkubwa wa Tamasha hilo katika msimu huu wa
sikukuu za Pasaka za mwaka huu jijini Mwanza.
Fanuel amesema kuwa tamasha la Mwaka huu lina utofauti mkubwa na la Mwaka jana maana
maandalizi ya Mwaka huu yako vizuri na
pia yameanza mapema ili kuhakikisha
wanatoa burudani ambayo kila mtu atakayefika uwanjani hapo ataifurahia, katika
kumbukumbu ya kufufuka Mwokozi Yesu Kristo.
Amesema tamasha la mwaka huu litafanyika kwa siku mbili
mfululizo katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza tarehe ishirini mwezi wa nne na tarehe
ishirini na moja mwezi wa nne mwaka huu ambalo litakuwa tofauti sana na miaka yote iliopita
maana lenyewe litakuwa la siku mbili.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The Great Zone Enteratainment Bi. Masele
Malekela amesema kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa kubwa sana kutokana na
mialiko ya waimbaji wakubwa na wakipekee wa Muziki wa Injili ambao hawajawi kufanya huduma Mwanza.
“Mwaka huwa tumejipanga vizuri sana kwa maandalizi makubwa ili kuwapa watazamaji na mashabiki wa matamasha yetu, tamasha kubwa na lenye
ubora na kiwango cha juu kitaifa”
Amewataja waimbaji kutoka Dar es salaam kuwa ni
Beatrice William wa BSS, Sheikh Jamal Jojo, Lusekelo Samwel, Chamwenyewe Jembe,
Jessica Julius, na kutoka Nzega Seiri Andrew, Kutoka Shinyanga Sarah Abel, na
Kutoka Mwanza Christina Victor, Rebeka Pius, Paulo Shole, Ajuaye Onesmo, Caphlen
Joseph.
Katika tamasha hilo la jumapili ya Pasaka kuna
uzinduzi wa Filamu mpya ya kikristo uitwayo Rafael ambayo imeigiziwa katika
jiji la Mwanza, pia siku hiyo kutakuwepo waimbaji wakali wa Muziki wa Injili
kusindikiza uzinduzi huo. Jumatatu ya Pasaka kuna mashindano ya kwaya ili
kupata mshindi wa kwanza ambaye atajinyakulia zawadi nzuri ili kumtia motisha
katika kazi ya uinjilishaji.
Tupe maoni yako