Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umesema kuwa
hautavumilia kuona wafanyakazi na wanachama wake wakivunja taratibu na kanuni
ilizojiwekea, kwa faida ya maslahi yao binafsi.
Hatua hiyo ya TFF imekuja ikiwa ni siku chache baada ya shirikisho
hilo kumlalamikia mfanyakazi wake mmoja katika Kamati ya Maadili kutokana na
kufanya udanganyifu katika suala la usajili wa mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel
Okwi.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
alisema kuwa siku zote wamekuwa wakiwataka watu kuzingatia taratibu na kanuni
za shirikisho hilo lakini baadhi yao wamekuwa wagumu kuzifuata.
“Kweli kabisa watu wamekuwa wakivunja taratibu na kanuni za TFF bila kujali.
Tupe maoni yako