Kocha Mkuu wa Simba,
Mcrotia Zdravko Logarusic, amesema iwapo ataendelea kukinoa kikosi hicho msimu
ujao, ndoto ya usajili wake ni kuchota nyota kutoka Ligi Kuu ya Kenya, kwani
kuna wachezaji wenye uwezo mzuri na wenye kuendana na weledi wa kisoka
(professionalism).
Loga ambaye aliwahi
kufundisha soka nchini humo akiwa na Klabu ya Gor Mahia, alisema Tanzania
imebarikiwa kuwa na vipaji vya soka lakini hawana weledi, ndiyo maana wanampa
tabu kufundisha.
Alienda mbali na kusema
kuwa katika kipindi alichokaa Tanzania, hajaona mchezaji mwenye uwezo wa
kucheza ligi kubwa hasa Ulaya kulinganisha na Wakenya waliosambaa kila kona ya
dunia.
“Wachezaji wa Kenya ni
waelevu, wanaelewa nini kocha anachotaka tofauti na hapa. Ndiyo, Tanzania kuna
vipaji, lakini wachezaji wake siyo welevu, ndiyo maana wananisumbua hata katika
ufundishaji.
“Kama kweli nitakuwa hapa
msimu ujao, nitaleta wengine kutoka kule,” alisema Loga huku akiisifia Gor
Mahia kuwa ina wachezaji wazuri.
Tupe maoni yako