Wandishi wa habari wakijadiliana juu ya tukio hilo huku wakiweka kumbukumbu kwa yale yanayopaswa kuwafikia walaji wa habari aka jamii. |
This is Skylight Beach Resort. |
MWANZA.
KITUO kipya cha Burudani cha Skylight
Beach Resort, kilichopo Sweya Kata ya Mkolani Wilayani Nyamagana kuzinduliwa rasmi
siku ya Wapendanao (Valentines Day) kwa Tamasha kubwa la burudani ya ufukweni mwa
mwambao wa Ziwa Victoria Jijini hapa.
Kufunguliwa kwa kituo hiki ni moja kati ya hatua za kuitikia wito wa serikali kwa wazalendo kuwekeza katika sekta ya utalii na burudani kwenye maeneo mbalimbali ya Majiji , Manispaa na Halmashauri za Wilaya.
Akizungumza na waandishi wa habari
Jijini humo jana, Mmoja wa Wakurugenzi wa Skylight beach Haruna Said alisema
kwamba, Kituo hicho kilichojengwa kwa hadhi ya Kimataifa na chenye madhari
nzuri ambacho kwa sasa ni gumzo na cha kwanza kwa ubora Jijini hapa.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kabla ya ufunguzi wa Ukumbi wa burudani wa Disko kuanza wamejipanga kuanza kutoa burudani ya ufukweni maarufu Foolmoon Beach Part ambayo itakuwa inafanyika kila mwezi mara moja kwa lengo la kutambulisha bidhaa mbalimbali zitakazopatikana Skylight Beach Resort.
Tupe maoni yako