MGOMO wa Madereva na Makondakta katika jiji la Mwanza leo umesababisha adha kubwa ya Usafiri hadi kuepelekea abiria kupanda bajaj, pickup na magari ya mizigo ili waweze kufika makazini na maeneo waliyotaka kwenda.
Mgomo huo ambao umeanza leo asubuhi umejuisha Daladala za ruti ya Ilemela Mahakamani via Kishiri na Daladala za Buhongwa via Igoma na, Buhongwa via ilemela.
Chanzo cha mgomo huu ni kituo cha kishusha na kupakia abiria kilichopo Buzuruga ambacho kimejengwa na Tanroads Mwanza kwa ajili ya kazi hiyo.
Wakiongea na Mtandao wa www.matukiomedia.blogspot.com madereva waliogoma wamelalamikia kituo hicho kuwa ni kidogo na pia hakikidhi mahitaji yao.
Aidha pia wamelalamikia baadhi ya Askari wa usalama barbarani kwa kukiuka taratibu za jeshi hilo kwa kuwakatama wengine bila kuwa na kosa la msingi.
Mwenyekiti wa Chama cha madereva kanda ya ziwa Bw: Dede Petro amesema kuwa madai yao yamelalamika siku nyingi lakini serikali imekuwa haiyazingatii mpaka imepelekea wagome leo.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali Meneja Tanroads Mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonad Kadashi amesema kuwa madai ya madereva hao ni ya msingi na ameota wiki moja kituoa hicho kirekebishe haraka iwezekanavyo.
Abiria wakiwa wamepakizwa katika moja kati ya pickup ambazo leo zimepata mwanya wa kupiga tripu katika jiji la Mwanza kuokoa adha ya usafiri ambayo imesababishwa na Daladala kugoma.
Hili gari limezimika kutokana na hitilafu katika mitambo yake.Hapa dereva amelipa first aid ili lipone mapema liendelee na shughuli kubwa na usafirishaji wa abiria.
Baadhi ya Daladala zikiwa zimepaki katika eneo la bustani ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga leo kama zilivyonaswa na kamera yetu ya www.matukiomedia.blogspot.com
Madereva wa Daladala wakionekana pichani mara baada ya kuongea na Afisa Mfawidhi ya Mamlaka ya Usarifi wa nchi kavu na majini Sumatra Japhet Ole Simaye kuusu mgomo wao.
Hichi ndicho kituo cha Buzuruga ambacho kinalalamikiwa na Madereva wa Daladala kuwa ni kidogo na hakikidhi mahitaji yao mpaka kipanuliwe ili magari yaweze kuingia na kutoka bila bugudha yoyote.
Kusanyiko la Kutafuta usuluhishi wa tatizo hilo likiendelea.
Afisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Ziwa Eng: Japhet Ole Simaye akitoa maelekezo kwa moja ya barua kutoka Sumatra kuhusu malalamiko ya Madereva wa Daladala waliogoma leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Kanda ya Ziwa Victoria Drivers Association Dede Boniventura Petro akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusu mgomo huu wa Madereva wake.
Meneja Tanroads Mwanza Eng: Leonard Kadashi akizungumzia hatma ya mgomo ambao umeanza leo wa Daladala na nini kifanyike maana kituo kilichojengwa na idara yake ya Tanroads ndio kimezua matata..
Madereva wakisikilizia upepo unavyokwenda kuhusu malalamiko yao.
Baadhi ya maafisa kutoka Serikalini na Tanroads wakitafuta mwafaka ili madereva waanze kusafirisha abiria ambao leo wamekionja cha moto kwa Daladala kugoma.
Huu ni msingi wa Kituo hicho cha magari cha Buzuruga ambacho kimejengwa kama kimeanza kutumika kama wiki moja. Hapa kimeanza kuharibika, swali je kikimaliza mwezi itakuwaje.
Mtaro amabo unapitisha maji machafu katika kituo hicho cha magari ya Daladala cha Buzuruga. Huu ni uchafu umeanza kutupwa humo, nini hatma yake.
Hili ni gari la Kampuni ya Lakairo Investment likawa limekwama katika round about barabara ya Kenyatta Road karibu na Hotel ya Goldcrest na kusababisha jam kubwa ya magari siku ya leo jijini Mwanza.
Hapa ndipo magari ya Daladala yanapita katika kituo kipya kushusha na kupakia cha Buzuruga kikianza kuleta nyufa kubwa. Kituo hiki kina takribani wiki moja toka kimeanza kutumika.
Tupe maoni yako