banner

.

.

Sunday, 16 February 2014

KONGAMANO LA DIVINE HERITAGE LAFANA KATIKA HOTEL YA MIDLAND JIJINI MWANZA...

KONGAMANO La Divine Heritage ambalo limefanyika leo katika Jiji la Mwanza, limefana sana kutokana na mamia ya watu kuhudhuria katika Kongamano hilo. 

Kongamano limeanza saa 8 mchana hadi 12 ambalo ambapo waalimu watatu ambao ni Pst Goodluck Kyara, Pst Denis Sebastian Kiandika na Pst Bill Brown wamefundisha somo la URITHI WETU KATIKA MUNGU.

Wakifundisha kwa nyakati tofauti Watumishi hao wa Mungu wamesema imefikia hatua wakristo wakubali kuuchukua urithi wao kwa Mungu maana ameshautoa tayari.
Wamesema wakrsito wengi wamesahau kuchukua urithi wao, na hivyo kuishi maisha ambayo sina wa watoto wa Mungu.

Wakitolea mfano wa wazazi wetu wa hapa duniani wanaandaa urithi kwa kila mtoto, Mungu wetu ni zaidi ya baba zetu wa duniani kutupa urithi mwema ambao hauharibiki.

Pia waimbaji mbalimbali kutoka Tafes Saut, Cbci Band, New Creation Band na mwimbaji binafsi Epafrodito wameimba na kusifu kwa kiwango cha juu mpaka uwepo wa Mungu ukashuka.
















Tupe maoni yako