Joel Maduka
Mwanza.
KANISA la aic igoma mwishoni
mwa wiki iliyopita lilibariki na kufungisha ndoa kumi na sita. Wachungaji waliohusika katika kufungisha
ndoa hizo ni wachungaji watatu wakiongozwa na mchungaji kiongozi Michael
Balele.
Mchungaji Balele aliwataka wanandoa hao kuishi
maisha ya upendo na kuchukuliana kwa madhaifu yote katika kipindi chote cha
ndoa na maisha yao.
Kwa upande wa wanandoa hao bw,Msadiki Kimaro amesema
kuwa ni vyema kwa wao kama wanandoa kupendana na kuvumiliana kwa mambo yote
muhimu ikiwa ni pamoja na kuombana msamaha na kupendana kwani upendo ni tunda
la roho.
Wakati huo huo
Kanisa la aic igoma Mwanza pia limewaweka wakfu wazee na wahudumu wa kanisa
kwaajili ya kufanya kazi ya utumishi wa mungu.
Katika ibada hiyo
iliyongozwa na wachungaji watatu chini ya mchungaji kiongozi mch,Michael
Balele,Henry Kanyumi na Jacob Ngaraba.
Mch: Jacob Ngaraba
amewataka waumini kuwapenda na kuwaombea viongozi waliochaguliwa kwa
kuwapa moyo na kushirikiana katika mambo
yote ya kiutumishi.
Kwa upande wake mzee wa kanisa Steven Shiringi,amesema
kuwa ni vyema kumtumikia mungu kwa
uwaminifu na amelitaka kanisa kuwaombea katika kazi zao za kikanisa.
Aidha bw,Msadiki Kimaro amesema kuwa kwa upande wake
ni vyema kwa viongozi wa makanisa wakatambua wito wao kwa kujitoa kwaajili ya
kumtumikia mungu. Jumla ya wazee wa kanisa 20 na wahudumu wa kanisa 10
waliwekewa mikono kwa siku kwa lengo la kutumikia kazi ya Mungu.
Tupe maoni yako