banner

.

.

Friday, 7 February 2014

CHAMA CHA CCM MKOA WA SHINYANGA YALAANI VURUGU ZA CHADEMA KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI KAHAMA.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Khamis M. Mgeja akimpa pole Afisa Mtendaji wa kata ya Ubagwe katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu Alphonce John Kimario aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na mapanga na watu aliowataja kuwa ni wafuasi wa CHADEMA, kupitia vurugu zilizotokea juzi saa moja usiku katika kata ya Ubagwe muda mfupi baada ya kumalizika kwa kampeni za kumnadi mgombea wao Bw. Hamisi Majogolo, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Itabola A. 
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa huyo Mtendaji wa kata ya Ubagwe, Alphonce John Kimario amesimulia kuwa sanjari na kuumia vibaya machoni hasa jicho lake la kulia pia analalamika juu ya maumivu makali anayo yasikia mgongoni mara baada ya kupigwa na nondo ambapo kwa hivi sasa upande wa kulia sanjari na bega lake umekufa ganzi. 
Ndugu Alphonce Kimario (Afisa Mtendaji wa kata ya Ubagwe) ambaye amepigwa nondo, amepigwa mapanga kwenye paji la uso kiasi cha kushonwa nyuzi kadhaa na kutobolewa jicho moja amekimbizwa hospitali ya Rufaa Bugando kutokana na hali yeke kuwa mbaya zaidi.
Tabitha Shuli ambaye ni Afisa Muuguzi Idara ya Macho Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza akimhudumia Ndugu Alphonce Kimario.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis M. Mgeja akiongozana na makada wengine wa CCM mkoa wa Mwanza kuelekea ward nyingine kuwaona majeruhi wengine walio lazwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza mara baada ya kushambuliwa kwa mapanga pamoja na kuharibiwa mali zao mara baada ya kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga..
Dereva wa gari la CCM wilaya ya Kahama Charles Peter akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa mapanga wakati wa kampeni za udiwani wilayani humo.
Majeruhi wengine  kama Masoud Melimeli (katibu Mwenezi wa Wilaya) amebaki katika uangalizi wa Hospitali ya Wilaya akiwa na majeruhi wengine kama Ramadhani Salum (Umoja wa Vijana) na Mussa Daudi (Katibu Uchumi Kata ya Nyihogo) ambaye alilazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama na mara baada ya kuzidiwa leo asubuhi amepakiwa katika AMBULANCE kuwahishwa Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi. Ikitajwa kuwa yeye alipigwa nondo ya kifuani.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Khamis M. Mgeja akimpa pole Sebastian Masonga (Katibu UVCCM Kata ya Majengo) aliyepigwa nondo na hatimaye kuvunjwa mkono wa kushoto, kuliani ni mwenyeji wa msafara huo ulio tembelea hospitali hiyo, Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Mama Joyce Masunga.
Sebastian Masonga ambaye ni Katibu UVCCM Kata ya Majengo akisimulia juu ya tukio zima la kuvamiwa. 

Tupe maoni yako