Poziiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Naitwa Masele Hamis Malekela nimezaliwa miaka
ishirini iliyopita jijini Mwanza, Nimezaliwa katika familia ya watoto watano
nikiwa mtoto wa pili kuzaliwa na mtoto wa kike wa pekee katika familia ya
Bw&Bi Malekela Hamis Malekela .
Nimeanza kusoma elimu ya msingi mwaka 2001
katika shule ya msingi Buzuruga Mwanza. Mwaka 2007 nikahitimu na kuchaguliwa
kujiunga na Kangae Sekondary School Mwaka 2008. Mwaka 2011 nikamaliza kidato
cha nne.
Sikubahatika kuendelea na elimu ya juu hivyo
basi nikajiunga na chuo cha computer kilichopo jijini Mwanza Bilal
Computer Training centre baada ya
kumaliza course ya computer nilisomea graphics Desigining na kufanya kazi
katika studio moja jijini mwanza
inayojulikana kwa jina la Cosu Universal Studio na baadae kuamia katika Kampuni
ya The Great Zone Entertainment ambayo
ndio nipo nafanya kazi mpaka sasa kama Mkurugenzi Mtendaji, ambayo inayohusika
na mambo yote ya burudani kama kurekodi filamu, kuandaa matamasha mbalimbali na
kuibua, kuinua na kuendeleza vipaji vya wasanii mbalimbali.
Toka nikiwa shule ya msingi waalimu wangu
walianza kubaini kipaji changu cha uigizaji na mara kwa mara katika maigizo ya
shuleni nilikuwa napewa nafasi kubwa kuigiza kutokana na kuigiza mpaka
kuwasisimua waalimu pamoja na wanafunzi wenzangu.
Baadhi ya maigizo niliyoweza kuigiza ni kama ya kuwaaga wahitimu wa darasa la saba na maigizo
ya sikukuu ya watoto. Niliingia rasmi kwenye sanaa ya uigizaji mwezi wa saba
mwaka 2012 na kujiunga na Kundi la sanaa la The Great Zone Entertainment ambalo
liko chini ya Mkurugenzi Fabian Fanuel
ambapo katika kundi hilo baada ya kupatiwa mazoezi ya kutosha na pia
kufahamu uusika mbalimbali nilifanikiwa kushiriki katika filamu mbili kama mhusika
mkuu yaani stering, Filamu hizo ni KAGALA, Filamu ya RAFAEL ameshirikiana na Wana Simulizi Club ambazo zitatoka hivi karibuni.
“Filamu ya Kagala ni filamu niliyoiigiza
katika maandhari ya kitamaduni na ni nzuri kweli, pia Filamu ya Rafael ni
filamu ambayo nimeiigiza katika maandhari ya Kimungu. Waongozaji wa filamu
waliamua kunibadilisha uhusika kutokana na kipaji kikubwa nilichonacho na
sikubahatisha katika kile ambacho nimekifanya humo ndani.”
Naamini katika filamu hizo nimefanya vizuri
na kwa wale wote mashabiki na wapenzi wa filamu za kitanzania wanipokee,
naamini wao wana mchango mkubwa sana katika kuifanya sanaa iwe juu hususani
sanaa ya Mwanza. Naamini kupitia sapoti yao nitaleta mabadiliko makubwa katika
Tasnia hii ya filamu maana watu wengi wanaamini wasanii wakubwa ndo wanaweza
kufanya sanaa nzuri tofauti na sisi maunderground.
Filamu yetu mpya ya Rafael ambayo inatarajia
kuingia sokoni hivi karibuni ambayo kihalisia nimecheza kama mdogo wake na
Rafael, sehemu hiyo nimeitendea haki sana na mimi mwenyewe nilijishangaa
kutokana na uigizaji ambao nimeuonyesha humo ndani, kikubwa nilizingatia
maelekezo ya waalimu wangu pamoja na waongozaji filamu wetu ili kufikia hali
hiyo.
Tofauti na kipaji cha uigizaji pia nina
vipaji vingine kama kucheza mpira wa miguu, Mc, na ninaamini kuna hazina ya
vipaji vingine ambavyo zimo ndani yangu siku
moja vitaonekana hadharani. Pia kwa sasa naendelea kujifunza kuongoza,
kushuti na kuedit filamu.
Tupe maoni yako